Israel imezidisha mashambulio baada ya mapendekezo ya kusitisha mapigano kutibuka
Jeshi la Israel limesema kuwa limetoa onyo tena kwa wakaazi wa mashariki na kaskazni mwa Gaza kuondoka majumbani mwao kwani wanaendeleza mashambulizi zaidi.
Onyo hili linajiri wakati majaribio ya kusitisha mapigano katika eneo hilo la Palestina yakionekana kutibuka.
Taarifa zinazohusiana
Mashariki ya kati
Maafisa wa jeshi wamesema kuwa maeneo mengi yanayotumiwa kurusha maroketi kutoka Gaza yamelipuliwa huku kundi la Hamas likiendeleza mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel.
Habari za punde zasema mashambulizi hayo ya Israeli yamelenga na kupiga nyumba za viongozi wa juu wa Hamas Mahmoud al-Zahar, na pia ile ya waziri wa zamani wa usalama wa ndani ya nchi Fathi Hamad.
Mwanamme mmoja mu-Israeli ameripotiwa kufariki alipogongwa na magruneti ya Hamas alipokuwa amekwenda kuwapelekea chakula wanajeshi wa Israel walioko karibu na mpaka wa Gaza.
vifo vingi na majeruhi yametokea miongoni mwa raia wa wapestina
Zaidi wa Palestiniana 200 wamefariki katika mashambulio haya ya sasa, wengi wamejeruhiwa, huku majumba na miundombinu ya Gaza ikiwa imeharibiwa sana.
Israel inadai imelazimika kuongeza mashambulio kwani Hamas wamekataa majadiliano ya kidiplomasia.
Hata hivyo msemaji wa Hamas, Osama Hamdan, ameiambia BBC kuwa hawaiamini Israel na hivyo hawawezi kuzungumzia mpango wa Amani wanaousikia tu kupitia vyombo vya habari kwani mpango kama huo hauwezi kamwe kuwasaidia wa- Palestina.
Inasemekana mapendekezo hayo sasa yamewasilishwa rasmi na Hamas wamesema wako tayari kuyajadili.
Mashirika ya kutoa huduma za kibinadamu huko Gaza yanasema mashambulizi hayo ya Israeli yameharibu hata miundo mbinu ya maji na upungufu mkubwa maji unajiri.
Shirika la umoja wa mataifa la misaada linasema mfumo wa maji machafu haufanyi kazi kamwe na asilimia 90 ya maji yaliyoko si safi kwa matumizi ya binadamu.