6 wauawa katika mlipuko Nigeria

Mlipuko wa bomu Nigeria
Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 6 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Taarifa zinazohusiana
Nigeria
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.
'Mashambulio ya awali'
Rais Goodluck Jonathan alilazimika kufutilia mbali ziara yake mjini Chibok wiki jana kutokana na utovu wa usalama
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.
Previous
Next Post »